Marcos Alonso bado hajapigwa rungu na FA - Darajani 1905

Marcos Alonso bado hajapigwa rungu na FA

Share This

Nyota wa Chelsea, Marcos Alonso anakabiliwa na adhabu ya kufungiwa michezo mitatu kutoka kwa chama cha soka nchini Uingereza mara baada ya kufanyika uchunguzi wa kina juu ya tukio alilolifanya kwenye mchezo ambao timu yake ilipambana dhidi ya Southampton siku ya jumapili ya tarehe 15-Aprili ambapo alimchezea vibaya nyota wa Southampton, Shane Long.

Katika dakika ya 43 ya mchezo huo ndipo tukio hilo lilitokea na mwamuzi wa mchezo huo, Mike Dean alishindwa kushuhudia kilichotokea na kushindwa kutoa adhabu kwa nyota huyo raia wa Hispania. Lakini baada ya mchezo huo, kamati maalumu ya waamuzi watatu wastaafu walichunguza kwa karibu juu ya tukio hilo na kuhitimisha kwa kukubaliana kuwa nyota huyo alistahili kutolewa kwa kuonyeshwa kadi nyekundu.

Taarifa rasmi kutoka kwa kamati hiyo ya watu watatu walio chini ya chama cha soka cha FA kikatoa ripoti yake kikitoa adhabu kwa mhispania huyo kwa kumfungia michezo mitatu ambayo ni ya ligi kuu Uingereza miwili (dhidi ya Burnley na Swansea) na mchezo wa nusu fainali ya kombe la FA dhidi ya Southampton.

Lakini pia chama hicho kimetoa muda wa kupinga adhabu hiyo ambapo kimesema kama Chelsea au Marcos Alonso atakua hajaridhishwa na adhabu hiyo basi afike siku ya jumatano ya tarehe 18-Aprili muda wa saa 06:00 jioni (saa 18:00) kwenye ofisi za FA na kama malalamiko yakionekana yana mantiki basi adhabu hiyo inaweza kutenguliwa

No comments:

Post a Comment