Rasmi; Chelsea kucheza dhidi ya Arsenal kombe la mabingwa - Darajani 1905

Rasmi; Chelsea kucheza dhidi ya Arsenal kombe la mabingwa

Share This

Wiki iliyopita nilikuletea habari juu ya Chelsea kuthibitisha kushiriki michuano ya kombe la mabingwa wa kimataifa, International Champions Cup (ICC) ambalo hufanyika mara baada ya msimu kuisha na nikakutaarifu kuwa ratiba ya michezo hiyo itatolewa au kupangwa ndani ya wiki hii.

Na sasa ratiba kamili ya michezo hiyo tayari imeshatolewa buku Chelsea ikipangwa kukutana na klabu tatu ambazo ni Sevilla ya Hispania, Inter Milan ya Italia na Arsenal kutoka Uingereza.

Ratiba kamili;
°Chelsea vs Sevilla
Uwanja; PGE Norodowy
Mahali; Warsaw, Poland
Tarehe; 28-Julai

°Chelsea vs Inter Milan
Uwanja; Ullevi stadium
Mahali;Gothenburg, Sweden
Tarehe; 1-Agosti

°Chelsea vs Arsenal
Uwanja; Friends Arena
Mahali; Stockholm, Sweden
Tarehe; 4-Agosti

No comments:

Post a Comment