Boca Juniors yamfata mlinda mlango wa Chelsea - Darajani 1905

Boca Juniors yamfata mlinda mlango wa Chelsea

Share This

Klabu ya nchini Argentina, Boca Juniors inatajwa kuwa kwenye mipango ya kumsajili mlinda mlango nambari mbili wa Chelsea, Willy Caballero ambaye alijiunga na Chelsea akitokea Manchester city kwa usajili huru.

Klabu hiyo inayoshiriki ligi kuu nchini Argentina inatajwa kuwa tayari kumsajili mlinda mlango huyo ambaye ni raia wa Argentina, lakini tu kama ikishindwa kumshawishi mlinda mlango wa sasa wa Juventus, Gianluigi Buffon.

Inaaminika mlinda mlango huyo atakubali kujiunga na wababe hao wa Argentina ambapo huko ataweza kupata nafasi katika kikosi cha kwanza licha ya kuwepo taarifa kwamba Chelsea inayomtumia kama mbadala ikipanga kumpa mkataba wa mwaka mmoja zaidi.

No comments:

Post a Comment