Chelsea itashiriki michuano ya kombe la mabingwa wa kimataifa, International Champions Cup (ICC) kwa msimu wa tano mwaka huu, michuano ambayo Chelsea itaitumia kama sehemu ya michezo ya kujiandaa na msimu mpya wa 2018-2019 ambapo kwa kawaida michuano hiyo hufanyika mara baada ya msimu kuisha.
Na tayari ratiba ya michezo hiyo ishapangwa na ishatangazwa, ili kuipata ratiba kamili, bonyeza hapa
Katika shughuli fupi ya kutangazwa kwa ratiba hiyo kulihudhuriwa na baadhi ya viongozi wa klabu kadhaa zilizothibitisha kushiriki michuano hiyo huku kwa upande wa Chelsea iliwakirishwa na nyota wake wa zamani raia wa Ghana, Michael Essien ambaye kwa sasa anaitumikia klabu mojawapo ya nchini Indonesia.
Michael Essien ametuma ujumbe kupitia mtandao wa Instagram, akionyesha kufurahishwa kwake kwa kuchaguliwa kuiwakilisha klabu ya Chelsea kwenye uzinduzi wa michuano hiyo.
No comments:
Post a Comment