Nyota wa Chelsea, Marcos Alonso anatajwa kutakiwa na wababe wa nchini Hispania, Real Madrid na Barcelona ambazo zote zinatajwa kuhitaji huduma ya mlinzi huyo ambaye amekuwa na msimu mzuri klabuni Chelsea, lakini kama ikitokea mlinzi huyo akaondoka klabuni hapo basi Chelsea itaingia sokoni kumsaka mlinzi atakayeweza kuziba pengo la nyota huyo.
Chombo kimoja kinachoaminika cha nchini Ufaransa kimeripoti Chelsea inamsaka nyota wa PSG, Kurzawa ambaye anatazamiwa kuziba pengo la Marcos Alonso endapo nyota huyo ataondoka Chelsea na kujiunga na wababe wa Hispania.
Kuondoka kwa Marcos Alonso kutaifanya Chelsea ibaki kuwa na mchezaji mmoja wa nafasi ya ulinzi wa kushoto, Emerson Palmieri na hivyo atakosa mbadala ambapo hilo ndilo linawafanya Chelsea imsake Kurzawa ili aje kuwa mbadala wa nafasi iyo ya kushoto.
No comments:
Post a Comment