Chelsea yaingiza mmoja kwenye kikosi bora cha msimu - Darajani 1905

Chelsea yaingiza mmoja kwenye kikosi bora cha msimu

Share This

Chama kinachosimamia wanasoka wakulipwa nchini Uingereza, Professional Football Association (PFA) kimetangaza kikosi bora cha msimu wa 2017-2018 cha ligi kuu nchini Uingereza ambapo kwenye kikosi hicho ni mchezaji mmoja tu wa Chelsea amefanikiwa kuingia ambaye ni mlinzi na winga wa kushoto wa klabu hiyo, Marcos Alonso ambaye mpaka sasa ameshaichezea Chelsea michezo 31 ya ligi kuu na kuifungia magoli 6 huku akipendezesha na uwezo wake mkubwa ya kufunga mipira ya adhabu.

Marcos Alonso ambaye ametokea kwenye ukoo wa wanasoka ambapo babu yake alikuwa mwanasoka wa klabu ya Real Madrid na timu ya taifa ya Hispania wakati pia baba yake aliwai kutamba na klabu ya Barcelona na timu ya taifa ya Hispania anafanikiwa kuingia kwenye kikosi bora hicho cha msimu wa 2017-2018 huku akiwa mchezaji pekee kutoka Chelsea huku nyota wenzake kama N'Golo Kante na Eden Hazard wakishindwa kuingia kwenye kikosi hicho.

Kama unakumbukumbu vizuri, huu ni msimu bora kwa Marcos Alonso ambapo amefanikiwa kuchaguliwa kuichezea timu yake ya taifa ya Hispania kwa mara ya kwanza kutokana na uwezo wake mkubwa aliouonyesha katika michuano yote ambayo Chelsea imeshiriki.

No comments:

Post a Comment