Conte akana kugombana na Rudiger, na mengi aliyoyaongea kwenye mkutano hii leo - Darajani 1905

Conte akana kugombana na Rudiger, na mengi aliyoyaongea kwenye mkutano hii leo

Share This

Chelsea itashuka uwanjani hapo kesho, kucheza mchezo wake wa ligi kuu Uingereza dhidi ya Burnley kwenye uwanja wa Turf Moor, mchezo ambao Chelsea inahitaji ipate ushindi ili kujiweka sawa kwenye mbio zake za kuwania kufudhu kucheza michuano ya klabu bingwa Ulaya msimu ujao haswa ukizingatia mpinzani wake, Tottenham jana alikubali kupata sare ya 1-1 alipomenyana dhidi ya Brighton.

Mpaka sasa Chelsea imeachwa alama nane na Tottenham inayoshika nafasi ya nne, na kama ikifanikiwa kupata ushindi kwenye mchezo huo wa kesho ambao kiukweli ni mgumu haswa Burnley anapokua kwake basi pengo hilo la alama litapungua kutoka alama hizo nane mpaka kufikia alama tano.

Kuelekea kwenye mchezo huo, kocha Antonio Conte amefanya mkutano na waandishi wa habari hii leo akiulizwa mengi kuhusu mchezo huo na kwa jinsi gani anayatazamia mambo yanavyoendelea klabuni Chelsea na nje ya klabu.

Kocha huyo aliulizwa juu ya nini anakiongelea kuhusu klabu ya Manchester city ambao wametawazwa rasmi kuwa mabingwa wa ligi kuu hiyo ya nchini Uingereza na kocha huyo aliisifia klabu hiyo kwa kuonyesha ubora na kiwango cha hali ya juu kuhusu klabu hiyo huku akikiri na kusema wamestahili kuwa mabingwa na alipoulizwa kama anadhani kama klabu hiyo itaendeleza ubora wake kwa msimu ujao kocha huyo alisema anaamini watakua bora sio kwa ligi kuu tu ila hata kwa michuano ya klabu bingwa kutokana na kuwekeza kwao nguvu katika kujenga kikosi na kupambana kuwa bora.

Alipoulizwa juu ya mwenendo wa Chelsea na jinsi anavyofikiri katika kupambania nafasi ya kucheza klabu bingwa kwa msimu ujao, kocha huyo alielezea akisema Chelsea inatakiwa iendelee kupambana kwa nguvu na jitihada zote huku akisema haihitaji kukata tamaa japo pengo la alama ni kubwa lakini muhimu ni kupambana kwa hali mpaka mwisho.

Lakini pia aliulizwa juu ya kauli iliyotolewa na Antonio Rudiger mara baada ya mchezo dhidi ya West Ham, mchezo ulioisha kwa sare ya 1-1 ambapo mlinzi huyo alikosoa falsafa akihoji inakuwaje Chelsea inapambana sana kuongoza mchezo lakini baadae inaruhusu kusawazishiwa ambapo hilo lilitokea kwenye mchezo huo na kwenye mchezo uliofata mlinzi huyo hakuwepo kabisa hata kwenye benchi, kocha huyo alijibu akisema kwenye mchezo dhidi ya Southampton nyota huyo hakuwepo ni kutokana na mbinu za mchezo na hakuna baya lolote alilolizungumza nyota huyo raia huyo wa Ujerumani.

Alipoulizwa juu nani ataziba pengo la Marcos Alonso kwenye mchezo huo wa kesho mara baada ya nyota huyo kufungiwa michezo mitatu. Kocha huyo alithibitisha kuwa Emerson Palmieri ndiye atatumika kwenye mchezo huo wa kesho kama mbadala wa Marcos Alonso.

Hayo ni baadhi ya aliyoyazungumza kocha wetu huyo kwenye mkutano wake wa leo alioufanya na waandishi wa habari.

No comments:

Post a Comment