Kocha Antonio Conte mchana wa leo alifanya mkutano na waandishi wa habari wakati Chelsea ikiwa inajiandaa kucheza mchezo wake wa ligi kuu Uingereza hapo kesho ambapo Chelsea itakuwa ugenini kucheza dhidi ya Burnley ambapo kama una kumbukumbu vyema mchezo huu ilitakiwa uchezwe toka mwezi Marchi ila ulihairishwa kutokana na ratiba ya mchezo huo na mchezo wa kombe la FA dhidi ya Leicester kubanana na hivyo mchezo huu ikabidi uupishe ule wa kombe la FA ambao Chelsea iliibamiza Leicester magoli 1-2 katika dakika 120 mara baada ya dakika tisini kuisha kwa sare ya 1-1.
Lakini wakati kocha huyo alipokuwa kwenye mkutano wake wa leo mchana kuna tukio lilitokea ambalo lilibaki kuwa kama kituko mara baada ya simu ya kocha huyo kuita akiwa anajibu maswali aliyoulizwa na waandishi wa habari.
Wakati mkutano huo ukiwa unaendelea ghafla simu ya kocha huyo iliita na ikabidi aombe radhi na kuamua kukata na kuizima na kuomba radhi kwa tukio hilo huku akisema ni mke wake ndio alimpigia lakini pia akisema mara zote mke wake huyo amekuwa akipiga wakati mbaya na baadae akatoa neno la utani huku akiishia kwa kuomba radhi.
No comments:
Post a Comment