Sarri azidi kuchangamkia fursa ya kumrithi Antonio Conte - Darajani 1905

Sarri azidi kuchangamkia fursa ya kumrithi Antonio Conte

Share This

Kocha wa sasa wa Chelsea, Antonio Conte haonekani kuendelea kusalia kuwa kocha wa klabu hiyo kwa msimu ujao haswa kutokana na Chelsea kuonekana kuwa na msimu mbaya ikishindwa kutetea taji lake la ligi kuu Uingereza lakini pia ikiwa na nafasi finyu ya kushiriki michuano ya klabu bingwa barani Ulaya huku akihusishwa kutakiwa na klabu ya nchini Ufaransa, klabu ya PSG.

Lakini wakati ikandaliwa mipango ya kocha huyo kuondoka, kocha Maurizzio Sarri ambaye ni kocha wa klabu ya Napoli ya nchini Italia ambayo ameiongoza vyema huku ikiwa nyuma ya walioko vileleni Juventus kwa alama sita ambapo kocha huyo amekuwa akitajwa kutakiwa na Chelsea amezua taarifa mpya kwa vyombo vya habari vya michezo vya barani Ulaya.

Vyombo vya habari vimekuja na taarifa zikisema kocha huyo anayesifiwa kwa uwezo wake mkubwa amekataa kuendelea kuwa kocha wa Napoli huku akidai anataka kuachana na klabu hiyo katika dirisha kubwa la usajili hali ambayo inafungua milango kwa Chelsea kumfata tena kocha huyo ambaye ilidaiwa amekubali kusaini mkataba wa kubaki Napoli.

Kocha huyo ana mkataba na Napoli unaoisha mwaka 2020 huku dau la kumsajili likiwa ni paundi milioni 7 alikuwa akidaiwa kuwa kwenye mazungumzo na rais wa Napoli ili asaini mkataba mpya na dau hilo la kuuzwa lifutiliwe mbali lakini sasa taarifa zinadai Chelsea ipo tayari kulipa dau hilo huku kocha huyo akiwa hapendelei kubaki klabuni hapo.

No comments:

Post a Comment