Usiku wa leo, Chelsea itakuwa ugenini kucheza mchezo wake wa ligi kuu Uingereza dhidi ya Burnley katika uwanja wa Turf Moor, uwanja ambao Chelsea iliondoka na alama moja msimu uliopita mara baada ya mchezo kuisha kwa suluhu ya 1-1.
Chelsea inashuka uwanjani hapo huku ikihitaji ipate ushindi ili kujiweka sawa kwenye msimamo wa ligi kuu Uingereza lakini pia ili kufufua matumaini mapya ya kurejea kwenye klabu nne za juu za msimamo wa ligi hiyo na kufanikiwa kuingia kwenye klabu zitakazoshiriki ligi ya mabingwa Ulaya.
Kuelekea kwenye mchezo huo, hapa nakuletea habari muhimu kuelekea kwenye mchezo huo wa ligi kuu.
Habari muhimu;
Chelsea; Emerson Palmieri anaenda kuichezea Chelsea mchezo wake wa kwanza wa ligi kuu Uingereza tangu asajiliwe na Chelsea akitokea As Roma ya Italia katika dirisha dogo la usajili la mwezi Januari. Emerson atatumika kama mbadala wa Marcos Alonso ambaye amefungiwa michezo mitatu na chama cha soka cha Uingereza mara baada ya kumchezea vibaya mshambuliaji wa Southampton, Shane Long kwenye mchezo uliopita.
David Luiz, Danny Drinkwater na Ethan Ampadu wote wataukosa mchezo wa leo kutokana na majeraha waliyokua nayo wakati Marcos Alonso nae ataukosa mchezo huo kutokana na sababu hiyo ya kufungiwa michezo hiyo mitatu.
Burnley; Ben Mee aliikosa michezo miwili iliyopita wakati Scott Arfield amekaa nje kwa miezi miwili sasa wote wataukosa mchezo wa leo kutokana na majeraha waliyokuwa nayo. Jon Walters tayari ameshapona majeraha yake aliyokuwa nayo lakini anahitaji muda zaidi wa kupona vizuri na kuwa sawa.
Mwamuzi; Robert Madley, ni mmoja kati ya waamuzi wadogo kwenye ligi kuu Uingereza ambapo kwa sasa ana miaka 32 huku takwimu zake kwa ligi kuu Uingereza msimu huu ameshakua mwamuzi kwenye michezo 29 huku akitoa kadi za njano 96 na kutoa kadi nyekundu 5.
Rekodi; Chelsea imepoteza mchezo mmoja tu kati ya michezo sita iliyocheza siku ya alhamisi katika michezo ya ligi kuu (Imeshinda michezo mitatu na kutoa suluhu michezo miwili)
Michezo iliyopita;
Chelsea: WLLDW
Burnley: WWWWW
Muda; Saa 09:45 Usiku (Saa 21:45) EAT
No comments:
Post a Comment