Kuelekea mchezo wa leo usiku, Conte atoa neno kuhusu Burnley - Darajani 1905

Kuelekea mchezo wa leo usiku, Conte atoa neno kuhusu Burnley

Share This

Chelsea inacheza dhidi ya Burnley usiku wa leo katika mchezo wa ligi kuu Uingereza kwenye uwanja wa Turf Moor (kupata habari muhimu kuhusu mchezo huu, bonyeza hapa). Mchezo ambao Chelsea ni lazima ipate ushindi ili kupunguza pengo la alama lililopo kati yake anayeshika nafasi ya tano na Tottenham inayoshika nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi kuu Uingereza kutoka alama nane mpaka kufikia alama tano.

Kuelekea kwenye mchezo huo, kocha Antonio Conte aliulizwa juu ya nini anakiona kipo tofauti kati ya nafasi yake kama kocha wa Chelsea na nafasi ya kocha wa klabu ya Burnley, Sean Dyche ambaye ameiongoza Burnley kushika nafasi ya saba kwenye msimamo wa ligi kuu huku wakishiriki ligi hiyo kwa msimu wa pili sasa tangu wapande kwenye ligi kuu msimu uliopita.

"Ni ngumu sana kufundisha Chelsea kuliko kuifundisha Burnley, ingawa Burnley ina fungu dogo kwenye usajili lakini kazi ya kuifundisha ni rahisi sana kuliko kuifundisha timu kama Chelsea inayohitaji kupata ushindi na mwisho ubingwa"

"Burnley inapambania kutokushuka daraja, ambapo hilo ndilo lengo lao kubwa na kama unavyofahamu, kushuka zinashuka timu tatu inamaana ukipambana kumaliza nafasi ya 16 hautoshuka lakini sio kama Chelsea ambayo yenyewe inataka kushinda kila mchezo na kuwa bingwa, na msimu utakua mbaya kwako maana ubingwa unabebwa na klabu moja na sio klabu tatu kama ilivyo kwenye kushuka daraja"

"Kwa michuano yote unayoshiriki kuna bingwa mmoja, na utaonekana sio kocha mzuri kama iyo uyo bingwa mmoja haitokua timu yako" alisema kocha huyo.

No comments:

Post a Comment