Kocha wa Chelsea, Antonio Conte haonekani kutamani kuendelea kuifundisha klabu hiyo ya Chelsea kwa msimu mwingine huku mkataba wake wa sasa ukiwa umebakiza mwaka mmoja. Unaisha mwaka 2019. Lakini pia bodi ya Chelsea nayo inatajwa kutotamani kuendelea kuipata huduma ya kocha huyo muitaliano huku chanzo kikubwa kikitajwa kuwa kocha huyo kutumia vyombo vya habari kulalamikia mfumo wa usajili ulivyo klabuni hapo ambapo inadaiwa hapendezwi mamlaka makubwa ya kuchagua wachezaji wa kuwasajili kuwa chini ya bodi badala ya kuwa chini yake kama kocha au mwalimu.
Kutokana na hali hiyo, televisheni ya Top Calcio ya nchini Italia iliripoti kuwa kocha huyo amepeleka maombi kwa klabu yake ya zamani ya Juventus kuwa anataka kurudi klabuni hapo ili aendeleze ufalme aliokuwa nao pindi alipokuwa hapo akishinda mfululizo mataji ya nchini humo lakini ikaripotiwa kuwa Juventus hawapo tayari kurudiana na kocha huyo
Lakini pia gazeti jengine lilidai kuwa Juventus yenye wasiwasi wa kumpoteza kocha wake Massimiliano Allegri ambaye anatajwa kutakiwa na klabu kadhaa kuwa inamtazamia aliyewai kuwa kocha msaidizi katika benchi la ufundi la klabu hiyo nyakati za kocha Antonio Conte, Massimo Carrera ambaye kwa sasa anaifundisha klabu ya Spartak Moscow kuwa ndiye mrithi wa Allegri kama ikitokea kocha huyo akaondoka.
No comments:
Post a Comment