Ampadu azidi kunogesha fainali ya Chelsea vs Arsenal usiku huu - Darajani 1905

Ampadu azidi kunogesha fainali ya Chelsea vs Arsenal usiku huu

Share This

Kikosi cha vijana wenye umri chini ya miaka 18 cha Chelsea, Chelsea U18s kinashuka uwanjani usiku huu wa leo ili kucheza mchezo wake wa fainali ya kwanza ya kombe la FA dhidi ya Arsenal ambapo fainali hiyo huwa na michezo miwili yaani nyumbani na ugenini, na safari hii Chelsea ipo nyumbani na itakuwa inaongozwa vyema na kocha Jody Morris.

Kuelekea katika fainali hiyo hapa nakuletea tukio ambalo labda hujalijua linaloongeza radha ingawa sio kwa ukamilifu.

Unajua ni tukio gani? ni tukio la vita ya mtu na mwanae ambapo mlinzi wa kikosi cha Chelsea, Ethan Ampadu atashuhudia kwa mara ya kwanza akiwa na upinzani na baba yake mzee  Kwame Ampadu. Kama ulikuwa haujui, mzee huyo, Kwame Ampadu ndiye kocha wa kikosi cha vijana cha Arsenal na usiku wa leo atakuwa pinzani wa mwanae ambae yupo Chelsea.

Lakini kama nilivyokwambia utamu hautokamilika kutokana na Ethan Ampadu kuwa na majeraha yanayomfanya kuukosa msimu huu kabisa. Kwa maana hiyo nyota huyo anaweza akaishia kuwa shabiki atakayeshuhudia klabu yake na klabu iliyochini ya baba yake zikimenyana.

No comments:

Post a Comment