Kocha wa Chelsea, Antonio Conte amefanya mkutano na waandishi wa habari katika kujiandaa kwake kucheza mchezo wa ligi kuu Uingereza dhidi ya Swansea mwishoni mwa wiki hii.
Kuelekea kwenye mchezo huo, hapa nakuletea alichokisema kocha huyo akiwa kwenye mkutano huo wa leo.
Alipoulizwa juu ya kama kuna majeruhi mapya klabuni hapo toka kucheza mchezo wa nusu fainali ya kombe la FA dhidi ya Southampton jumapili iliyopita, kocha huyo alisema "Hapana, hakuna majeruhi wapya".
Alipoulizwa juu ya David Luiz kama ataweza kurejea kucheza kwa msimu huu, kocha huyo alisema hana uhakika kama mchezaji huyo raia wa Brazil kama ataweza kurejea uwanjani msimu huu licha ya kuwa vyema kwenye mazoezi.
Alipoulizwa juu ya nafasi ya kinda Andreas Christensen ambapo amekuwa akitumika zaidi kwenye safu ya ulinzi ambapo nafasi yake kwa sasa inaonekana kutumika zaidi na Gary Cahill, kocha huyo amemsifia Cahill kwa kusema amekuwa akijitahidi kucheza nafasi hiyo ya ulinzi wa kati na anadhani ni wakati sahihi wa mwingereza huyo kutumika kama chaguo la kwanza.
Alipoulizwa juu ya nini anakiwaza kuelekea mchezo dhidi ya Swansea, kocha huyo amesema huo utakuwa mchezo mgumu maana itakuwa ni dhidi ya klabu inayopandana kutokushuka daraja lakini akasema kutokana na ubora wa Chelsea ni lazima ipambane na kuhakikisha inaondoka na alama tatu ili kuongeza presha kwa Tottenham kwenye kupambania kucheza klabu bingwa msimu ujao.
No comments:
Post a Comment