Klabu ya soka ya vijana wenye umri chini ya miaka 18, Chelsea U18s inafanikiwa kupata ushindi wake muhimu wa fainali ya kwanza ya kombe la FA ikiwa nyumbani Stamford Bridge na kufanikiwa kuiadhibu klabu inayofundishwa na baba wa nyota wa Chelsea Ethan Ampadu, mzee Kwame Ampadu ambaye anaifundisha Arsenal iliyopoteza usiku wa kuamkia leo kwa kipigo cha mabao 3-1.
Arsenal ndio walikuwa wa kwanza kupata goli la kuongoza ambapo walipata goli la kwanza katika dakika ya 36 ya kipindi cha kwanza na kuufanya mchezo kwenda mapumziko huku Chelsea ikiwa nyuma kwa goli 0-1.
Kipindi cha pili kilianza na ndipo kocha Jody Morris wa kikosi hicho cha vijana ambapo alimuingiza Daishawn Redan ambaye ndiye alikuwa shujaa wa mchezo huo ambapo mnamo dakika ya 67 nz kufanya matokeo kusomeka sare ya 1-1 lakini baada ya robo saa kufika, Guehi akatumia uwezo wake mkubwa kuipatia Chelsea goli la pili wakati goli la tatu na la mwisho lilifungwa tena na Daishawn Redan ambaye alilifunga saa 86. Na kuifanya Chelsea iondoke na ushindi huo wa mabao 3-1.
Kwa matokeo hayo, sasa Chelsea itahitaji kupata suluhu au ushindi wowote ili kuweza kulitwaa taji la kombe la FA ambapo mchezo wa marudiano utachezwa siku ya tarehe 30-Aprili
No comments:
Post a Comment