Antonio Conte atoa majibu kuondoka Chelsea - Darajani 1905

Antonio Conte atoa majibu kuondoka Chelsea

Share This

Kocha wa Chelsea, Antonio Conte ambaye amekuwa akihusishwa kuondoka klabuni hapo ifikapo mwishoni mwa msimu haswa kutokana na inavyotaarifiwa kuwa ana mahusiano mabovu na bodi ya klabu hiyo juu ya maswala ya usajili klabuni hapo.

Kocha huyo aliyebakisha mwaka mmoja na miezi miwili kwenye mkataba wake wa sasa unaoisha mwaka 2019 ametoa majibu juu ya kutakiwa na klabu ya nchini Ufaransa, klabu ya PSG inayotazamia kuachana na kocha wake Unai Emery ambaye anaonekana hana maisha marefu kwenye klabu hiyo.

Kocha Conte ambaye ni raia wa Italia, jana alitoa majibu alipoulizwa kuhusishwa kwake kutakiwa na klabu hiyo na kipi anakitazama kuhusu maisha yake klabuni Chelsea.

"Hapana (hakuna kinachoendelea kwangu na PSG). Swali hili nimekuwa nikilibu sana kwamba kwa sasa hakuna naloliwaza zaidi ya Chelsea" alisema kocha huyo.

No comments:

Post a Comment