ROBO FAINALI YA KOMBE LA FA YAPANGWA - Darajani 1905

ROBO FAINALI YA KOMBE LA FA YAPANGWA

Share This

Droo ya kombe la FA kwa hatua ya robo fainali imechezeshwa leo usiku, huku ikisimamiwa na magwiji wa soka, Michael Owen akiwa na mlinda mlango wa zamani aliyewai kutamba na klabu ya Mama site (Man city), Shay Given ambapo kwa hatua hiyo ya robo fainali, Chelsea imepangwa kucheza dhidi ya Leicester city, ambapo mchezo wa kwanza utachezwa kwenye uwanja wa Leicester maarufu kama King Power Stadium.

Droo hiyo imepangwa muda mfupi uliopita na Chelsea kupangiwa vigogo hao wanaoongozwa na kocha Claude Puel, ambaye aliwai kumfundisha Eden Hazard pindi walipokuwa kwenye klabu ya nchini Ufaransa, klabu ya Lille.

Michezo ya hatua hiyo ya robo fainali inaweza kuchezwa tarehe 16 mpaka tarehe 19 ya mwezi Marchi.

Michezo mingine;
°Sheffield Wednesday/Swansea vs Rochdale/Tottenham
°Manchester United vs Brighton
°Wigan/Manchester City vs Southampton
NB; Alama ya "/" inaonyesha mmojawapo kati yao, imekuwa ivo kutokana na michezo yao kutokuchezwa bado.

No comments:

Post a Comment