CHELSEA YAKUBALI KUMUUZA BATSHUAYI, ILA KWA MASHARTI - Darajani 1905

CHELSEA YAKUBALI KUMUUZA BATSHUAYI, ILA KWA MASHARTI

Share This

Nyota wa Chelsea, Michy Batshuayi aliyepo kwa mkopo kwenye klabu ya nchini Ujerumani, Borrusia Dortmund, na amekuwa na msimu mzuri na uwezo mkubwa sana klabuni hapo akifunga magoli matano huku akitengeneza jengine moja kwa kutoa pasi ya mwisho, akifanya hivo katika michezo mitatu tu kuichezea klabu hiyo toka kusajiliwa kwa mkopo na klabu hiyo katika dirisha dogo la mwezi Januari ambapo atakuwa klabuni hapo mpaka mwishoni mwa msimu.

Kutokana na uwezo mkubwa aliouonyesha klabuni hapo ameonekana kuwa mrithi sahihi kwa klabu hiyo mara baada ya kumpoteza mshambuliaji wake, Pierre Aubameyang aliyejiunga na klabu y Arsenyanii (Arsenal).

Kwa taarifa zilizopo, zinadai kuwa Chelsea inaweza kubadili msimamo wake wa kutotaka kumuuza mchezaji huyo ili aendelee kubaki Dortmund, kama klabu hiyo itakubali kumruhusu nyota wake raia wa Marekani, Christian Pulisic ajiunge na Chelsea.

Mwanzoni kulitoka taarifa kuwa Chelsea haitazamii kumuuza Michy Batshuayi ili ajiunge na klabu hiyo lakini Chelsea imeamua kubadili mawazo na badala yake itamruhusu mbelgiji huyo ajiunge na klabu hiyo kwa sharti la Dortmund ikubali kumuachia Pulisic ajiunge na Chelsea.

No comments:

Post a Comment