Sababu 3 zilizoifanya Chelsea kumkosa Michael Seri - Darajani 1905

Sababu 3 zilizoifanya Chelsea kumkosa Michael Seri

Share This

Nyota raia wa Ivory Coast aliyekuwa anafukuziwa na Chelsea pamoja na Arsenal, Jean Michael Seri amejiunga na klabu ya Fulham ya nchini Uingereza kwa usajili ulioigharimu Fulham paundi milioni 18.

Nyota huyo mwenye miaka 26 amekamilisha usajili huo aliosaini miaka minne na kujiunga rasmi na klabu hiyo inayoshiriki ligi kuu Uingereza kuanzia msimu wa 2018-2019 mara baada ya kufanikiwa kufudhu kucheza michuano hiyo kwa kuifunga Aston Villa katika mchezo wa kukamilisha timu tatu zitakazocheza ligi kuu Uingereza kwa msimu ujao.

Seri amekuwa akitajwa kwa karibu kutua Chelsea, lakini kwanini usajili wake wa kutua Chelsea umeshindwa kukamilika?

Sababu #1
Klabu ya Chelsea imekuwa na msuguano unaotajwa kuendelea chini kwa chini juu ya bodi yake na kocha wa klabu hiyo hivyo kuwepo fununu za kocha Antonio Conte kufukuzwa klabuni hapo, lakini hilo limeshindwa kukamilika mpaka sasa na kusababisha kutokueleweka kama kocha huyo ataendelea kuifundisha klabu hiyo kwa msimu ujao au ataajiriwa kocha mpya. Sababu hiyo ya kutokujulikana nani atakuwa kocha wa klabu hiyo kwa msimu ujao kumemfanya Seri kuamuqa kujiunga na Fulham.

Sababu #2
Kutokuwa na uhakika wa nafasi kwenye kikosi cha kwanza. Uchezaji wake unafanana na N'Golo Kante klabuni Chelsea hivyo kumfanya kuwa na hofu ya kucheza kwenye kikosi cha kwanza. Haitazamiki kama kocha atakuwa na nafasi ya kuwachezesha wote wawili lazima mmoja aanze na mwengine asubiri benchi.

Sababu #3
Chelsea kutokuonyesha nia ya kumtaka. Kulikuwa na tetesi tu kwamba Chelsea inamtaka lakini klabu hiyo haikuonyesha nia ya dhati ya kumtaka nyota huyo, aliwai kunukuliwa wakala wa nyota huyo akisema nyota huyo atachagua timu ya kwenda kutokana na klabu hiyo kuonyesha nia ya dhati ya kuhitaji huduma ya nyota huyo.

Kupata habari zote za Chelsea, tembelea kurasa zetu
Facebook➡Darajani 1905
Instagram➡darajani1905

No comments:

Post a Comment