Chelsea ilimsajili akitokea nchini kwao Brazil kwenye klabu ya Fluminense na sasa imekamilisha kumtoa kwa mkopo kwa mara ya pili akitimkia kulekule alipokua msimu uliopita, Newcastle United ambayo nayo inashiriki ligi kuu Uingereza pamoja na Chelsea.
Kennedy Robert, nyota raia wa Brazil aliyepewa jina hilo na wazazi wake kutokana na wazazi hao kupendezwa na kiongozi na mwanasiasa wa zamani wa nchi ya Marekani, Robert F. Kennedy amekamilisha uhamisho wake wa mkopo wa kujiunga na klabu ya Newcastle united aliyoitumikia nusu ya msimu uliopita akijiunga nayo kwenye dirisha dogo la usajili la mwezi Januari akimpisha nyota mwenzake raia wa Italia mwenye asili ya Brazil, Emerson Palmieri aliyesajiliwa akitokea klabu ya As Roma ya nchini Italia.
Kennedy anayejulikana kwa uwezo wake wa kupiga vyenga na kuuchezea mpira kama ilivyo desturi ya nyota wenye asili ya Brazil amekamilisha usajili huo wa mkopo wa mwaka mmoja atakapoitumikia klabu hiyo itakayokuwa na ruksa ya kumsajili kwa usajili wa moja kwa moja ifikapo mwishoni mwa msimu.
Newcastle iliyonusurika kushuka daraja msimu uliopita huku kazi kubwa ikifanywa na nyota huyo imekuwa ikimfukuzia nyota huyo ili imsajili kwa usajili wa jumla lakini Chelsea imekuwa ikipinga jambo hilo kutokea.
Kupata habari zote za Chelsea, tembelea kurasa zetu
Facebook➡Darajani 1905
Instagram➡darajani1905
No comments:
Post a Comment