"I am the coach of series" unayakumbuka maneno hayo? aliyaongea kocha Antonio Conte muda mfupi baada ya kuisaidia Chelsea kushinda taji la Kombe la FA pale Wembley stadium mwezi May mwaka huu akimaanisha yeye ni kocha wa mfululizo yaani kushinda mataji kwake anashinda mfululizo. Alianza kuipa Chelsea taji la ligi kuu Uingereza katika msimu wake wa kwanza kufika klabuni hapo na msimu wake wa pili akaiwezesha kushinda taji la Kombe la FA ambalo kwa Uingereza lina thamani kubwa kutokana na historia yake.
Lakini leo hii kumetangazwa au kuripotiwa habari kwamba kocha huyo ameachana rasmi na Chelsea huku akiwa amebakiza mkataba wa mwaka mmoja wa kuendelea kuifundisha klabu hiyo.
Gazeti la nchini Italia, Sky Italia limeripoti kutimuliwa kwa kocha huyo raia wa Italia aliyedumu klabuni hapo kwa misimu miwili kabla ya hii leo kuripotiwa kwa habari hiyo ambayo inawagawa mashabiki wa Chelsea katika mafungu wengine wakipongeza lakini wengine wakihuzunishwa na taarifa hizo zinazokuja muda mfupi tangu kocha huyo arejee klabuni rasmi kuiandaa klabu kucheza michezo ya kirafiki ya kujiandaa na msimu mpya ambao Chelsea itashiriki michuano minne ambayo ni ligi kuu Uingereza, ligi ya Ulaya (Europa League), Kombe la FA na kombe la ligi.
Je wewe umehuzunishwa au umependezwa na taarifa hii?
Kupata habari zote za Chelsea, tembelea kurasa zetu
Facebook➡Darajani 1905
Instagram➡darajani1905
No comments:
Post a Comment