Bado usajili wake haujatangazwa rasmi kwamba umekamilika, lakini kwa hali ilivyo ni kama tayari Chelsea imefanikiwa kumnasa nyota huyo raia wa Italia mwenye asili ya Brazil.
Ni Jorginho anayetajwa kukaribia kabisa kuwa mchezaji wa Chelsea katika dirisha hili kubwa la usajili na hilo amelionyesha wazi kutokana na majibu yake wakati alipohojiwa na moja ya vyombo vya habari.
"Ni ngumu kwangu kuondoka Napoli, mji wake nimeshauzoea na itakuwa ngumu kwangu kupasau." alisema nyota huyo
Kauli hiyo inatafsiriwa kwamba tayari ameshasaini klabuni Chelsea na kubwa alichobakiza ni kutangazwa rasmi huku ikielezwa amepewa mkataba wa miaka minne wenye thamani ya paundi 102,000 kwa wiki klabuni Chelsea.
Kupata habari zote za Chelsea, tembelea kurasa zetu
Facebook➡Darajani 1905
Instagram➡darajani1905
No comments:
Post a Comment