Sasa ni rasmi kwamba kocha Antonio Conte hatoendelea kuifundisha klabu ya Chelsea kwa msimu ujao licha ya kocha huyo kubakisha mkataba wa mwaka mmoja wa kuifundisha klabu hiyo.
Na taarifa hizo zimemfikia pia nyota wa zamani wa Chelsea na timu ya taifa ya Uingereza, John Terry ambaye ametumia mtandao wa Instagram kumuaga kocha huyo ambaye walifanya kazi kwa pamoja kwa msimu mmoja kabla ya Terry kuondoka Chelsea na kujiunga na klabu ya Aston Villa.
Terry ametuma ujumbe mfupi kumtakia mema kocha huyo raia wa Italia ambaye mpaka anaondoka Chelsea ameisaidia klabu hiyo kushinda mataji mawili.
John Terry kwasasa hana timu anayoichezea na amekuwa akifika kwenye viwanja vya mazoezi vya Chelsea akifanya mazoezi ili kujiweka sawa.
Kupata habari zote za Chelsea, tembelea kurasa zetu
Facebook➡Darajani 1905
Instagram➡darajani1905
No comments:
Post a Comment