Barcelona yaifata tena Chelsea - Darajani 1905

Barcelona yaifata tena Chelsea

Share This

Mwanzoni walikuja na paundi milioni 50 ili kumsajili nyota wa Chelsea, Willian Borges lakini Chelsea ikakataa dau hilo lakini sasa kuna taarifa kwamba klabu hiyo ya Barcelona imeandaa dau jipya ili kumsajili nyota huyo.

Barcelona wanatajwa kutenga dau la paundi milioni 53 ili kumnasa winga huyo raia wa Brazil mwenye miaka 29

Taarifa zinazoripotiwa ni  kwamba klabu hiyo ya Barcelona inayoshiriki ligi kuu nchini Hispania imekuja na dau hilo huku kukidhaniwa mazungumzo yanaendelea kati ya klabu hizo ili kukamilisha usajili huo huku kukitaarifiwa pia kwamba Chelsea inataka paundi milioni 72.

Kupata habari zote za Chelsea, tembelea kurasa zetu
Facebook➡Darajani 1905
Instagram➡darajani1905

No comments:

Post a Comment