Chelsea kuwanasa wawili kutoka Napoli - Darajani 1905

Chelsea kuwanasa wawili kutoka Napoli

Share This

Kuondoka kwa kocha Antonio Conte kunamaanisha Chelsea ipo sokoni kumsaka kocha mpya na tetesi zilivyo inaelezwa kocha wa klabu ya Napoli, Maurizzio Sarri ndiye atakuwa mrithi wa nafasi hiyo klabuni Chelsea.

Maurizzio Sarri mwenye miaka 59 ambaye msimu uliopita aliiwezesha klabu ya Napoli kumaliza nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi kuu nchini Italia anatajwa kuwa mrithi wa kocha Antonio Conte haswa kutokana na maneno yaliyozungumzwa na rais wa klabu ya Napoli akisema wanasheria wake pamoja na wanasheria wa Maurizzio Sarri wapo kwenye mazungumzo ya kukamilisha kuondoka kwa kocha huyo.

Lakini kuna taarifa zinazoaminika kwamba kocha huyo anaondoka na nyota wa Napoli, Jorginho ambaye picha zilizosambaa mitandaoni zinamuonyesha akiwa anafanyiwa matibabu kujiandaa kutua Chelsea.

Dau la paundi milioni 51 linatajwa kuwajumuisha nyota hao wawili ambapo Chelsea inatumia dau hilo kuwanasa Sarri na Jorginho kwa pamoja.

Kupata habari zote za Chelsea, tembelea kurasa zetu
Facebook➡Darajani 1905
Instagram➡darajani1905

No comments:

Post a Comment