Rasmi; Maurizzio Sarri kocha mpya wa Chelsea - Darajani 1905

Rasmi; Maurizzio Sarri kocha mpya wa Chelsea

Share This

Hatimaye lile lililokuwa linasubiriwa kwa muda mrefu la kutangazwa kocha mpya wa Chelsea limekamilika mchana wa leo mara baada ya klabu hiyo inayopatikana magharibi-kusini mwa jiji la London kumtangaza kocha Maurizzio Sarri kuwa kocha mpya wa klabu hiyo.

Sarri ambaye amekuwa akihusishwa kwa muda mrefu kutakiwa na Chelsea licha ya vipingamizi vya hapa na pale kuibuka hatimaye amesaini mkataba mpya wa kuinoa Chelsea kwa miaka mitatu ambapo hiyo itamaanisha mkataba wake utamalizika mwaka 2021.

Maurizzio Sarri ambaye anasifika kwa mfumo wake wa kucheza pasi fupi za haraka anatarajiwa kuanza kazi ya kuifundisha Chelsea kuanzia sasa wakati klabu inapojiandaa kucheza michezo ya kirafiki kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa 2018-2019 huku akianza mchezo wa kirafiki kucheza dhidi ya Perthy Glory ya huko nchini Australia, mchezo utakaochezwa tarehe 23-Julai.

Lakini pia kama haujui, Maurizzio Sarri anatimiza idadi ya makocha watano waitaliano kuwai kuifundisha Chelsea ikiwa chini ya Roman Abramovich huku watangulizi wake wakiwa ni Claudio Ranieri, Carlo Ancellotti, Roberto di Matteo na Antonio Conte.

Karibu Darajani..

Kupata habari zote za Chelsea, tembelea kurasa zetu
Facebook➡Darajani 1905
Instagram➡darajani1905

No comments:

Post a Comment