Je ni Antonio Conte au Maurizzio Sarri? - Darajani 1905

Je ni Antonio Conte au Maurizzio Sarri?

Share This

Taarifa zilizopo zinadai kwamba kocha Maurizzio Sarri bado ana nafasi ya kuchukua mikoba ya kocha Antonio Conte klabuni Chelsea licha ya Conte kuendelea na mazoezi pamoja na nyota wa Chelsea ambao wanajiandaa kucheza mchezo wa kirafiki siku 12 zijazo huko nchini Australia.

Taarifa zilizoripotiwa kutoka kwa rais wa klabu ya Napoli, Aurelio zinadai kwamba wanasheria wa rais huyo wamekutana na wanasheria wa Maurizzio Sarri ili kukamilisha mambo yanayohitajika kabla ya kocha huyo kuachana na klabu hiyo iliyomteua kocha Carlo Ancellotti kuanza kuwa kocha huyo.

Sarri amekuwa akitajwa kurithi nafasi ya kocha Antonio Conte klabuni Chelsea licha ya kocha Antonio Conte kuamua kurejea klabuni hapo na kuendelea na majukumu yake.

Kukaribia kutua kwa kiungo Jorginho klabuni Chelsea akitokea Napoli kunafungua njia kwa Maurizzio Sarri kutua klabuni hapo muda wowote kuanzia sasa.

Je unamtaka Antonio Conte au Maurizzio Sarri? acha maoni yako hapo chini

Kupata habari zote za Chelsea, tembelea kurasa zetu
Facebook➡Darajani 1905
Instagram➡darajani1905

No comments:

Post a Comment