Kombe la Dunia; Gary Cahill, Loftus-Cheek kushuka uwanjani leo - Darajani 1905

Kombe la Dunia; Gary Cahill, Loftus-Cheek kushuka uwanjani leo

Share This

Wakati jana timu ya taifa ya Ufaransa ikifanikiwa kutinga fainali ya Kombe la Dunia huko nchini Urusi kwa ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Ubelgiji katika hatua ya nusu fainali, leo ni zamu ya Uingereza itakayokuwa uwanjani kumenyana dhidi ya Croatia.

Uingereza yenye nyota wawili wa Chelsea, Gary Cahill na Ruben Loftus-Cheek inacheza mchezo huo wa leo ili kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kushinda Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza ambapo kama ikifanikiwa kushinda mchezo wa leo itakutana dhidi ya Ufaransa yenye nyota wengine wawili kutoka Chelsea, N'Golo Kante na Olivier Giroud.

Mchezo huo wa nusu fainali utachezwa usiku wa leo mida ya saa 09:00 Usiku (Saa 21:00) kwa saa za Afrika Mashariki.

Kupata habari zote za Chelsea, tembelea kurasa zetu
Facebook➡Darajani 1905
Instagram➡darajani1905

No comments:

Post a Comment