Jorginho ni nani? - Darajani 1905

Bado haijatangazwa rasmi kwamba ni mchezaji mpya wa Chelsea lakini kutokana na maneno ya mmiliki wa klabu anayoichezea, Napoli kukiri kwamba biashara ya nyota huyo kutua Chelsea ni kama ishakamilika.

Ni usajili wa Jorginho kutua Chelsea. Hilo ndilo linalotawala kwasasa huko kwenye tovuti zinazoripoti habari za Chelsea.

Jorginho anatajwa kupanda ndege ili kufika nchini Uingereza ili kukamilisha usajili wake wa kutua Chelsea huku dau la paundi milioni 51 likitajwa kutumika kwenye usajili huyo.

Jorginho ni nani?
Jina lake kamili ni Jorge Luiz Frello Filho ni mchezaji raia wa Italia aliyezaliwa miaka 26 iliyopita huko nchini Brazil lakini alifika nchini Italia akiwa na miaka 15 ambapo huko alifanikiwa kupata uraia wa Italia kutokana na bibi na babu yake kuwa ni waitaliano.

Ni mchezaji wa aina gani?
Ni mchezaji anayecheza nafasi ya kiungo akitumika sana kama mchezaji kiungo mchezeshaji akiwa na uwezo mkubwa wa kupiga pasi na kutengeneza mashambulizi.

Historia yake kwa ufupi
Alianzia maisha yake ya soka akiwa kwenye klabu ya Hellas Verona ya nchini Italia kabla ya baadae kuuzwa kwenda Napoli ambapo huko amefanikiwa kuingia kwenye kikosi cha kwanza na kuitwa kwenye timu ya taifa ya Italia.

Nafasi yake klabuni Chelsea
Kutua kwake Chelsea kunamaanisha Chelsea itakuwa na viungo watano ambao ni Danny Drinkwater,  Cesc Fabregas, N'Golo Kante, Tiemoue Bakayoko na yeye Jorginho lakini ujio wake ni kama Chelsea inajiandaa na maisha mapya bila Fabregas ambaye amebakiza mkataba wa mwaka mmoja ambao unamalizika mwishoni mwa msimu huu.

Takwimu zake
Kwa msimu uliopita alicheza jumla ya michezo 41 huku akifunga magoli 3 na kutoa pasi za mwisho 4 lakini akiwa na uwezo wa kupiga pasi zinazofika kwa 89% wakati akipiga mashuti golini kwa wastani wa 0.5 huku akitoa pasi murua, pasi zinazofika kwa mchezo kwa wastani wa 1.5

Kupata habari zote za Chelsea, tembelea kurasa zetu
Facebook➡Darajani 1905
Instagram➡darajani1905

No comments:

Post a Comment