Majukumu ya uongozi klabuni Chelsea kwa nafasi ya unahodha kwa sasa yapo chini ya muingereza Gary Cahill ambaye ameyapokea majukumu hayo kutoka kwa mkongwe wa Chelsea ambaye nii mwingereza mwenzake, John Terry ambaye mwenyewe aliondoka Chelsea msimu uliopita mara baada ya kuwa hapo kwa miaka 22.
Nahodha Cahill ametoa neno kuelekea mchezo wa jumatatu ambapo Chelsea itakuwa uwanjani kupambana dhidi ya West Bromwich Albion katika uwanja wa Stamford Bridge, ambapo mchezo huo unakuja mara baada ya juma lililopita kupoteza mchezo katika uwanja huohuo dhidi ya Afc Bournemouth.
"Michezo miwili iliyopita hatukucheza vizuri. Kama wachezaji , na naamini hata kwa upande wa kocha , tunachokiamini na tunachokipigania ni kucheza vizuri na kurejea kwenye ubora wetu katika mchezo unaokuja siku ya jumatatu"
"Kama ukiangalia historia ya klabu hii kwa miaka kumi iliyopita, tumekuwa na mafanikio makubwa sana. Tumepata matokeo mazuri na ni kama tuliwashangaza wengi kwa makubwa tuliyofikia. Hivyo ndivyo klabu hii imekuwa kwa miaka yote toka nimekuwa hapa. Napenda kuwashukuru mashabiki kwa kutuamini kwa vipindi vyotem maana kwa sehemu ya tisa kati ya kumi wamekuwa nyuma yetu na kutupatia nguvu ya kupambana. Sitarajii kuona tukiwaangusha mashabiki wetu, nachokiona kuwa bado tuna nafasi ya kufanya makubwa na kuwashangaza wengi kama tulivyokuwa tunafanya kwa miaka yote" alisema Cahill.
Chelsea itacheza jumatatu dhidi ya West Bromwich ambapo itahitaji ushindi katika mchezo huo ili irejee katika nafasi nne za juu mara baada ya kushushwa na Tottenham ambao wamepata ushindi katika mchezo wao wa leo dhidi ya Arsenyani (Arsenal)

No comments:
Post a Comment