Chelsea imetajwa kuelekea kukamilisha mazungumzo na kocha wa zamani wa Barcelona, Luis Enrique ili kuchukua nafasi ya kocha wa sasa wa Chelsea, Antonio Conte anayepewa nafasi kubwa ya kuondoka klabuni hapo huku ikielezwa anaweza kuondoka Chelsea ifikapo mwisho wa msimu huu.
Luis Enrique anatajwa kukubali kutua Chelsea, ingawa masharti yake anataka kutua hapo mwisho wa msimu na sio katikati ya msimu kama ilivyokuwa inatajwa na wengi.
Lakini sasa klabu ya Arsenyani (Arsenal) inatajwa kuhusishwa kuingilia Chelsea katika kumuwania kocha huyo ambapo taarifa zinadai kuwa Arsenyani inamhitaji kocha huyo ili kuchukua mikoba ya Arsene Wenger ambaye anatajwa kuhusishwa kuachana na klabu hiyo mwishoni mwa msimu huu.
Je Arsenyani watafanikiwa kuipokonya Chelsea kocha huyo aliye mapumzikoni kwa sasa?
No comments:
Post a Comment