Chelsea inatajwa kuwa klabu ya mwisho kutoa ofa nene na nzito ya kumnasa nyota na kiungo wa klabu ya Aston Villa, Jack Glealish ya nchini Uingereza iliyoshindwa kushiriki ligi kuu msimu ujao mara baada ya kupoteza mbele ya Fulham kwenye mchezo wa fainali ya kugombania kushiriki ligi kuu (play-off final).
Chelsea inatajwa kuwa tayari kutoa paundi milioni 30 ili kumsajili nyota huyo anayetaka kuachana na klabu hiyo mara baada ya kushindwa kufudhu lakini mashabiki wa Chelsea wanatajwa kuupinga usajili huu.
Unajua kwanini? Mashabiki hao wanaamini kiwango cha nyota huyo hakina ukubwa huo wa kutisha na ni mara mia Chelsea iwatumie makinda wake Mason Mount pamoja na Callum Hudson-Odoi ambao wote wana vipaji vya kuweza kuisaidia Chelsea na sio kupoteza pesa zake kwenda kumsajili jamaa huyo mwenye miaka 22.
No comments:
Post a Comment