DROGBA ARUDISHA FURAHA NCHINI KWAO - Darajani 1905

DROGBA ARUDISHA FURAHA NCHINI KWAO

Share This
Nyota wa zamani wa Chelsea, Didier Drogba ambaye kwa sasa anamiliki klabu ya Phoenix akiwa kama mmoja wa wamiliki wa klabu hiyo lakini pia akiwa mchezaji wa klabu hiyo ametengeneza shule nchini kwao Ivory Coast katika moja ya vitongoji alivyowai kutokea nchini humo.

Kupitia taasisi yake ya Didier Drogba Foundation ametengeneza shule hiyo a msingi katika kitongoji hicho na kutuma ujumbe wa kuonyesha kufurahishwa na mafanikio hayo aliyoyafikia.

Didier Drogba atakumbukwa vyema na wana Iory Coast kama mmoja wa nyota na mashujaa nchini humo ambapo kama haujajua alishawai kuhusika kwenye kusimamisha vita ya wenyewe kwa wenyewe nchini huko ambapo alituma ujumbe akiwa kama nahodha wa timu ya taifa kwa wananchi wa Ivory Coast akiwaomba kusimamisha vita.

Kupitia mtandao wa Instagram, Drogba alituma ujumbe akisema "Nina furaha sana kufanikiwa kujenga shule na kubadilisha hali ya watoto wa kijiji hiki cha Onario Pokou Koumaekro. Kuweza kuwapatia mazingira mazuri na elimu bora maana elimu. Nataka kuliona tabasamu hili katika nyuso zao siku zote za maisha yangu. Asante kwa shirikiano wa @nestle na I'ICI"

No comments:

Post a Comment