ANTONIO CONTE AMKOSA MSHAMBULIAJI - Darajani 1905

ANTONIO CONTE AMKOSA MSHAMBULIAJI

Share This
Kocha wa Chelsea, Antonio Conte aliwai kumuwania nyota raia wa Ghana ambaye anacheza nafasi ya ushambuliaji Richmond Boakye katika dirisha la usajili lililopita, lakini usajili huo ukaonekana kushindikana mara baada ya Chelsea kuhusishwa kwa karibuni na mshambuliaji raia wa Bosnia, Edin Dzeko ambaye pia baadae walimkosa na kufanikiwa kumnasa Olivier Giroud kutoka Arsenyani (Arsenal).

Mara baada ya kuachana na mshambuliaji huyo raia wa Ghana ambaye ilikuwa inaelezwa alikuwa ni pendekezo la kocha Antonio Conte, nyota huyo amekamilisha usajili wake wa kujiunga na klabu ya Jiangsu suning inayoshiriki ligi kuu nchini China kwa usajili wa dau la euro milioni 5.5 (Tanzania shilingi billioni 15) na kufaikiwa kusaini mkataba wa miaka mitatu klabuni hapo. Nyota huyo alikuwa akiichezea klabu ya Red Star Belgrade ambaye kwa sasa ana miaka 25.

No comments:

Post a Comment