KITAMBO; UNAIKUMBUKA HII? CHELSEA KWENYE UWANJA WA MABARAFU - Darajani 1905

KITAMBO; UNAIKUMBUKA HII? CHELSEA KWENYE UWANJA WA MABARAFU

Share This
Kama utakuwa mfuatiliaji mzuri kwenye mitandao ya kijamii, nadhani utakuwa umeshashuhudia wachezaji wa Chelsea wakituma picha na video kuonyesha hali ilivyo kwa sasa nchini Uingereza ambapo kumekuwa na hali ya kudondoka kama mvua ya mabarafu (snow) ambayo hutokea katika kipindi cha majira ya baridi. Wachezaji wengi wametuma picha na video juu ya tukio hilo, David Zappacosta, Tiemoue Bakayoko, David Luiz na wengine wametuma ujumbe huo.

Lakini leo nataka nikukukmbushe kitu fulani, sidhani kama utakuwa unakumbuka au hata unalijua tukio hili, lakini usijali nipo hapa ili kukujuza.

Unakumbuka tarehe 23-Oktoba-1997 kilitokea nini kilichoihusisha Chelsea?
Sidhani kama utakuwa unakumbuka. Chelsea ilikuwa ugenini huko kwenye nchi ya Norway ambapo ilifika huko kucheza mchezo wake wa muhimu katika kombe la washindi (Cup Winners' cup) dhidi ya klabu wababe wa nchi hiyo, Tromso ambao wenyewe kiasili ilianzishwa miaka 15 mara baada ya Chelsea kuanzishwa, Chelsea ilianzishwa mwaka 1905 wakati klabu hiyo ilianzishwa mwaka 1920.

Chelsea ilifika uwanjani kwao ikiwa na nyota kadhaa kama Ruud Gullit, Gianluca Vialli, Dennis Wise, Gianfranco Zola na Roerto di Matteo. Sasa nini nataka kukumbusha katika mchezo huu.

Mara baada ya Chelsea kuruhusu kufungwa magoli ya haraka ambapo ndani ya dakika 20 tayari ilishafungwa magoli 2-0, ghafla mvua ya mabarafu (snow) ikaanza kushuka. Mwanzoni haikuonekana tatizo sana, lakini baadae ikazidi mpaka kufikia hatua ule ukijani wa uwanja kutoonekana kabisa na badala yake wachezaji wakawa wanakanyaga lile barafu. Mchezo ulisimamishwa mara mbili ili wasafisha uwanja wapitishe mifagio maalumu katika sehemu ya uwanja, ila sio sehemu zote, kwenye ile mistari ya uwanja inayoonyesha eneo la uwanja kisha mchezo ukawa unaendelea.

Ulikuwa mchezo wa kushangaza maana ilitegemewa kwa jinsi hali ilivyokuwa mbaya basi mchezo ungesimamishwa, lakini hilo halikutokea na badala yake mchezo ukaamrishwa uendelee. Mpaka leo mashabiki wengi wa soka wanashangazwa na tukio kama lile la kuendelea kwa mchezo wakati hali ya hewa ilikuwa mbaya, na mwisho wa siku mchezo ukaisha kwa Tromso kushinda 3-2.

Lakini katika mchezo wa marudiano ambao ulichezeka Stamford Bridge huku Chelsea wakiwa nyumbani wakiwakaribisha Tromso, Chelsea haikutaka kuleta mzaha mbele ya mashabiki wake na wakaibamiza klabu hiyo magoli 7-1 na kufanya matokeo kumalizika kwa Chelsea kushinda ushindi wa jumla wa mabao 9-4 na kufanikiwa kufudhu kucheza hatua nyengine. Msimu huohuo walifanikiwa kuibamiza Real Madrid katika mchezo wa fainali ya Uefa Super cup kwa goli 1-0 na kuibuka kuwa mabingwa.

No comments:

Post a Comment