KUMBUKUMBU YA MFALME WA STAMFORD BRIDGE, JE ULIKUWA UNAIJUA HII? - Darajani 1905

KUMBUKUMBU YA MFALME WA STAMFORD BRIDGE, JE ULIKUWA UNAIJUA HII?

Share This

Bila shaka mtu akikuuliza umtaje mfalme wa Stamford Bridge utamtaja John Terry kutokana na makubwa aliyoyafanya klabuni Chelsea akiichezea kwa miaka 22 na kufanikiwa kuwa nahodha aliyeshinda mataji mengi nchini Uingereza kwa kushinda mataji matano ya ligi kuu akiwa kama nahodha raia wa Uingereza, lakini nataka nikurekebishe, pamoja na ukubwa wake, lakini nyota huyo sio mfalme wa Stamford Bridge.

Mfalme wa Stamford Bridge alishafariki miaka 12 iliyopita, ambapo leo ndio anatimiza miaka 12 toka kufariki kwake. Tarehe 1-Marchi-2006 ndio ilikuwa siku aliyofariki mfalme wa Stamford Bridge ambaye alitengeneza heshima kubwa klabuni hapo mpaka kufikia kuitwa kwake kuwa mfalme wa Stamford Bridge, uwanja wene historia kubwa nchini Uingereza uliojengwa mwaka 1877.
Peter Osgood (wa pili kutoka kushoto) akiwa studio na wachezaji wenzake

Nani ni mfalme wa Stamford Bridge? mfalme wa Stamford Bridge ni gwiji wa soka wa zamani ambaye alikuwa ni raia wa Uingereza, Peter Osgood aliyeichezea Chelsea kwa mafanikio makubwa kwa vipindi viwili tofauti. Kama utakuwa na kumbukumbu vizuri nilishawai kukuletea makala yake fupi kuhusu gwiji huyo ambaye kwa sasa ni marehemu katika kumbukumbu ya siku yake ya kuzaliwa. Kusoma historia hiyo bonyeza hapa.
Peter Osgood (mstari wa juu wa tatu kutoka kulia) wakiwa studio wakirekodi

Sasa leo sitaki nikukumbushe mengi kuhusu gwiji huyo ambaye kwa sasa ni hayati, ila kuna jambo moja nataka nikujuze kama ulikuwa hujui. Unaijua ile nyimbo maalumu ya Chelsea? yani ndio kama nyimbo ya utambulisho ya Chelsea, huwa inaimbwa "Blue is the colour, football is the game. We're all together and winning is our aim" nadhani wengi wetu tunaijua, na kama unataka kuipakua (download) basi bonyeza hapa chini
https://www.dropbox.com/s/d0fqy7xs63mh3rl/%28Hdvidz.in%29_Chelsea-FC-Anthem-Song---Blue-Is-The-Colour-With-Lyrics-bY-b0Ld.mp4?dl=0
Unajua kama Osgood alihusika kwenye wimbo huo? ndio alihusika. Gwiji huyo aliyekuwa akicheza kama mshambuliaji aliungana na wachezaji wenzake wa Chelsea kwa miaka hiyo na kufika studio ambapo huko walirekodi nyimbo hiyo kwa mara ya kwanza na kufanikiwa kutolewa mwaka 1972. Nyimbo hiyo ilitamba sana mpaka kufikia hatua kuvunja rekodi mbalimbali kutokana na kuhusisha wanasoka katika nyimbo hiyo.

Peter Osgood leo anatimiza miaka 12 toka kufariki kwake dunia, na amepewa heshima kubwa klabuni Chelsea mpaka kufikia hatua sanamu yake kuwekwa katika uwanja wa Chelsea nyuma ya jukwaa la The Shed End, jukwaa maarufu zaidi klabuni hapo.

No comments:

Post a Comment