Willian aeleza angefanya nini kama Kocha Conte angebaki Chelsea - Darajani 1905

Willian aeleza angefanya nini kama Kocha Conte angebaki Chelsea

Share This

Chelsea kwasasa ipo chini ya kocha Maurizio Sarri, aliyechukua nafasi ya kocha Antonio Conte ambaye aliachishwa kazi siku kadhaa toka alipoanza mazoezi ya kujiandaa na msimu mpya akitokea mazoezini.

Nyota wa Chelsea, Willian Borges ambaye amekuwa akihusishwa kwa karibu kutaka kuondoka klabuni hapo huku kisa kikitajwa kutokuwa na mahusiano mazuri na kocha huyo aliyeisaidia Chelsea kushinda mataji mawili ndani ya misimu miwili alipokuwa kocha wa Chelsea, nyota huyo amefanyiwa mahojiano na kuulizwa kama angebaki endapo Chelsea isingeamua kumtimua Conte, winga huyo alijibu akisema

"Kiukweli hapana. Ingekuwa ngumu kwangu kubaki. Lakini kama klabu ingeamua kuniuza, basi nami ningeondoka" alisema winga huyo raia wa Brazil ambaye siku kadhaa zilizopita alisheherekea kutimiza miaka 30 toka kuzaliwa kwake.

Willian alikuwa sehemu ya kikosi cha Chelsea kilichopata ushindi katika mchezo wa kwanza wa ligi kuu Uingereza kwa msimu wa 2018-2019 ambapo Chelsea ilimenyana dhidi ya Huddersfield na kuishuhudia ikiondoka na ushindi wa magoli 0-3 huku Willian akitoa pasi ya goli la kwanza lililofungwa na N'Golo Kante.

No comments:

Post a Comment