Ligi kuu Uingereza kwa vijana wa akademi ilianza hapo jana kwa upande wa klabu ya vijana ya Chelsea maarufu kama Chelsea U23's ambapo jana walicheza mchezo wao wa kwanza kwa kucheza dhidi ya klabu ya vijana ya Everton (Everton U23's) na kufanikiwa kuondoka na alama moja mara baada ya matokeo ya suluhu ya 1-1.
Chelsea U23s ilikuwa nyuma kwa goli 0-1 kabla ya Charly Musonda Jr kusawazisha kwa mkwaju wa penati katika dakika ya 69' na kufanya matokeo kuwa sare ya 1-1 dhidi ya klabu hiyo ya vijana ya Everton.
Kutokana na matokeo hayo, klabu hiyo ya vijana inafanikiwa kufikisha alama moja ikiwa nafasi ya pili katika msimamo wa kundi la kwanza (Premier League 2 standing group 1)
No comments:
Post a Comment