Rasmi; Bakayoko akamilisha uhamisho wa kuondoka Chelsea - Darajani 1905

Rasmi; Bakayoko akamilisha uhamisho wa kuondoka Chelsea

Share This

Nyota na kiungo wa Chelsea, Tiemoue Bakayoko amekamilisha uhamisho wa kujiunga kwa mkopo na klabu ya AC Milan iliyokuwa ikimfukuzia kwa muda mrefu.

Bakayoko ambaye alijiunga na Chelsea kwenye dirisha kubwa la mwaka 2017 alitua Chelsea akitokea klabu ya AS Monaco.

Chelsea imeweka kipengele cha paundi milioni 36 ambapo kama AC Milan ikitaka kumsajili jumla basi ni lazima walipe dau hilo ili kumnasa mfaransa huyo.

Kusajiliwa kwa viungo kama Jorginho Frello na Mateo Kovacic na kubakishwa kwa kiungo Ruben Loftus-Cheek kunafanya nafasi ya Bakayoko kuzidi kufifia kwenye kikosi cha kocha Maurizio Sarri.

No comments:

Post a Comment