Batshuayi atambulishwa rasmi, atoa neno kuhusu kutolewa kwa mkopo - Darajani 1905

Batshuayi atambulishwa rasmi, atoa neno kuhusu kutolewa kwa mkopo

Share This

Nyota wa Chelsea, Michy Batshuayi ambaye ni nyota raia wa Ubelgiji amekamilisha uhamisho wa mkopo wa kujiunga na klabu ya Valencia CF inayoshiriki ligi kuu nchini Hispania.

Mara baada ya uhamisho wake kukamilika, nyota huyo ametambulishwa rasmi hii leo na uongozi wa klabu hiyo ya Valencia ambapo ametoa neno kuhusu kujiunga mkopo na klabu hiyo.

"Kulikuwa kuna klabu kadhaa zilizotaka kunisajili, lakini nilipoongea na Marcelino (kocha wa Valencia) nikaona kuna kitu tunaendana kuhusu mimi nayeye."

"Hii ni timu inayoshiriki klabu bingwa Ulaya, itapambana dhidi ya klabu bora. Nategemea kufanya makubwa nikiwa hapa. Lakini kubwa lililonishawishi nifike hapa ni kutokana na maongezi yangu na kocha Marcelino" alisema nyota Michy Batshuayi.

Batshuayi alisajiliwa na Chelsea akitokea klabu ya Olympique Marseille ya nchini Ufaransa na msimu uliopita alitumika akiwa kwa mkopo akiwa klabuni Borrusia Dortmund.

No comments:

Post a Comment