Moja kati ya wachezaji ambao klabu ya Chelsea imekuwa ikilalamikiwa kwa kumruhusu aondoke ni Nemanja Matic tena haswa lawama zinakuja kwa kuwa ameuzwa kwa klabu pinzani, klabu ya Manchester united ambako huko ndiko alipo kocha wa zamani wa Chelsea, Jose Mourinho ambaye alifanikiwa kuungana tena na mchezaji huyo ambaye waliwai kushinda pamoja taji la ligi kuu Uingereza mwaka 2015 pindi walipokua Chelsea katika dirisha kubwa la usajili lililopita.
Wachambuzi wengi wa soka wamekuwa wakisema Chelsea itajutia kwa kumruhusu mserbia huyo akaungana na klabu hiyo, lakini je unajua haswa sababu iliyomfanya akaondoka Chelsea? kocha wa Manchester united, Jose Mourinho ameamua kuvunja ukimya na kueleza haswa sababu gani ilimfanya nyota huyo akaachana na Chelsea na kujiunga na Man utd.
"Matic ni mchezaji mzuri. Mwezi Marchi-2017 aliniambia ni lazima aichezee Man utd, maana anataka kuwa chini yangu, na kweli akalitimiza lile alilolisema" alisema kocha huyo raia wa Ureno.
Kwa kauli hii ya Mourinho inaeleza kuwa Matic hakuwa na furaha na maelewano mazuri akiwa chini ya kocha Antonio Conte japo haikuwai kujulikana hivyo hapo kabla, na aliitumikia vyema klabu hiyo mpaka kufanikiwa kushinda taji la ligi kuu Uingereza akiwa na kocha huyo klabuni Chelsea kwa msimu uliopita.
Mwezi Februari mwaka huu wakati Chelsea ilipokuwa inajiandaa kumenyana dhidi ya Manchester united, kocha Antonio Conte aliulizwa juu kujiandaa kwake kumenyana dhidi ya nyota wake huyo wa zamani ambapo aliishia kusema kuwa ni mchezaji mzuri lakini alikataa kuzungumzia zaidi kuhusu nyota huyo akisema hakuna haja ya kuyazungumzia yaliyopita maana hayana maana kwa muda huo.
No comments:
Post a Comment