Kante kutakiwa na PSG, Chelsea yataja dau inalotaka ili kumuuza - Darajani 1905

Kante kutakiwa na PSG, Chelsea yataja dau inalotaka ili kumuuza

Share This

Chombo cha habari cha nchini Ufaransa maarufu kama RMC kimeripoti juu ya taarifa za nyota wa Chelsea, N'Golo Kante ambaye anatajwa kuhusishwa na klabu ya PSG kutoka nchini Ufaransa.

Chombo hicho cha habari kimeripoti kuwa Chelsea imetaja dau la paundi milioni 88 (euro milioni 100) kama kuna klabu itatokea na kumtaka nyota huyo aliyejiunga na Chelsea akitokea Leicester city kwa dau la paundi milioni 35 lakini pia chombo hicho kinadai kuwa kiungo huyo anataka kuendelea kubaki Chelsea na hatazamii kuondoka klabuni hapo.

Ripoti hiyo inazidi kuchimbua na kusema moja ya viongozi wa klabu ya PSG amekuwa akifanya mawasiliano na wawakilishi wa kiungo huyo ingawa nyota huyo amekataa kuondoka na inaaminika klabu hiyo ya PSG inamtafuta mrithi wa kiungo wake, Thiago Motta ambaye umri wake unaonekana kuutupa mkono soka la ushindani na hivyo kumtaka Kante ili kuziba pengo la kiungo huyo.

No comments:

Post a Comment