Chelsea inatajwa kuingia kwenye vita ya kumnasa mlinzi wa klabu ya Arsenal raia wa Hispania, Hector Bellerin anayetajwa kutakiwa pia na klabu za Barcelona, Manchester united na Juventus.
Chelsea inatajwa kumtaka nyota huyo mwenye miaka 23 ambaye anatajwa kutaka kuachana na klabu hiyo ifikapo mwishoni mwa msimu huu ambapo anataka kujiunga kwenye klabu yenye kushindania mataji na kuwa katika nafasi nzuri katika kupambania mataji.
Kocha wa klabu hiyo, Arsene Wenger ametangaza kuachana na klabu hiyo ifikapo mwishoni mwa msimu na nyota huyo anatajwa kutokua tayari kusalia klabuni hapo.
No comments:
Post a Comment