Klabu ya Chelsea inatajwa kuingia kwenye mpango wa kumnasa nyota raia wa Ufaransa anayeichezea klabu ya Manchester united, Anthony Martial ambaye amekataa kusaini mkataba mpya wa kusalia kwenye klabu hiyo inayofundishwa na kocha wa zamani wa Chelsea, Jose Mourinho.
Chelsea inatajwa kuwa kwenye mipango ya kukimbia adhabu ya masuala ya kiuchumi na biashara yenye usawa kisoka maarufu kama Financial Fair Play ambapo inaweza ikakutana na adhabu hiyo endapo itashindwa kufudhu kucheza klabu bingwa msimu ujao na kama ikishindwa ishawaandaa wachezaji ambao italazimika iwauze ili kuendana na sheria hiyo ambapo kati ya hao kuna na Eden Hazard na hivyo kuifanya Chelsea imuhitaji zaidi Anthony Martial ili aje ajaribu kuziba pengo la mbelgiji huyo. Kusoma orodha kamili ya wachezaji wanaoweza kuuzwa, bonyeza hapa
Chelsea inatajwa kumtaka winga huyo anayetajwa kutakiwa pia na klabu kadhaa barani Ulaya huku Chelsea ikiingia kwa nia kubwa ili kumnasa.
No comments:
Post a Comment