Klabu ya Chelsea inapambana kupata nafasi ya kushiriki michuano ya klabu bingwa Ulaya kwa msimu ujao. Imebakiza michezo mitatu ya ligi kuu Uingereza ili kupambania nafasi hiyo, na kama ikishindwa kufudhu kucheza michuano hiyo basi itakosa fungu la kuanzia paundi milioni 70 kutokana na kushindwa kucheza michuano hiyo.
Hali hiyo inatajwa kuiweka klabu hiyo katika hatari ya kupigwa rungu juu ya sheria ya za usajili wa uwiano sawa maarufu kama Financial Fair Play ambapo ili kuendana na sheria hiyo klabu hiyo inatajwa kuingia kwenye ulazima wa kuwauza wachezaji wake tisa ili iepuke rungu au adhabu hiyo.
Eden Hazard anatajwa kuwepo kwenye kundi hilo na thamani yake inatajwa kufikia paundi milioni 100 lakini pia nyota wengine ni pamoja na David Luiz ambaye anatakiwa na Napoli na As Monaco, Danny Drinkwater, Michy Batshuayi ambaye Borrusia Dortmund wapo tayari kumnunua kwa paundi milioni 50, Kenedy anayeichezea kwa mkopo Newcastle anatajwa kuwa na thamani ya paundi milioni 20.
Marco van Ginkel na Lucas Piazon wote wanatajwa kuwa na thamani ya paundi milioni 10. Taarifa hii imeripotiwa na gazeti la The Telegraph.
No comments:
Post a Comment