Kocha wa Chelsea, Antonio Conte alifanikiwa kuinasa saini ya mlinzi kutoka klabu ya As Roma ya nchini Italia ambaye ni raia wa Ujerumani, Antonio Rudiger katika dirisha kubwa la usajili lililopita na sasa kocha huyo anatajwa kumtamani nyota mwengine kutoka nchini Ujerumani ambaye amekuwa akitajwa kama mrithi wa mlinzi wa zamani wa Ujerumani, Phillipe Lahm ambaye kwa sasa ameshastaafu soka.
Chelsea inatajwa kuandaa dau la paundi milioni 31 ili kumnasa mlinzi raia huyo wa Ujerumani anayeitwa Benjamin Henrichs na ni mlinzi wa klabu ya Bayer Leverkusen ya nchini kwao Ujerumani.
Benjamin Henrichs mwenye uwezo mkubwa wa kucheza kama mlinzi wa pembeni lakini pia akicheza kama mlinzi wa kati anatajwa pia kufukuziwa na klabu za jiji la Manchester ambazo ni Manchester united na Manchester city huku akizidi kuzitamanisha klabu nyingi haswa kutokana na umri wake wa miaka 21 lakini pia akionyesha uwezo mkubwa mpaka kuitwa Phillipe Lahm mpya huku akiichezea Bayer Leverkusen michezo 27 kwa msimu huu.
No comments:
Post a Comment