Maurizio Sarri baada ya kutua tu pale darajani kufuatia kuondoka kwa Muitaliano Antonio Conte alilitaja jina la Jorge Luiz Frello Filho (Jorginho) kuwa usajili wake wa kwanza kwenye dirisha hili la majira ya kiangazi kutoka SSC Napoli.
Sarri (the cigarette man) alijua anaenda shamba na hakuweza kuliacha jembe lake Jorginho, kwani angetumia nini kulimia?
Jorginho nilimshuhudia msimu uliopita akifanya kazi kubwa pale kati akishirikiana vyema na wenzie Allan, Marques Loureiro pamoja na Marek Hamšík nahodha wa klabu ya Napoli.
Jorginho ni kiungo mkabaji asiye tumia nguvu nyingi na jana tulimuona akisimama mbele ya walinzi na kazi yake kubwa ikiwa ni kuzuia mashambulizi.
Ujio wa wa kiungo huyu katika kikosi cha Chelsea kimemfanya Mfaransa N'golo Kante acheze juu zaidi kuliko chini.
Jorginho ambaye ndio mfungaji wa goli la pili Jana kwa mkwaju wa penati kati ya magoli 3 yaliofungwa na Chelsea na kuwapa alama 3 katika mchezo dhidi ya Huddersfield amekuwa na msaada mkubwa kwa kocha Sarri na muhimili mkubwa kwa mfumo anaoutumia kwani mfumo wa 4-3-3 unaitaji kiungo mkabaji wa kati (Central Defensive Midfielder) mtulivu ama mtu ambaye anauwezo wakufanya maamuzi kwa haraka huku akiwa na uwezo wa kuzuia pasi za wapinzani kiurahisi na kuanzisha mashambulizi kwa urahisi halikadhalika.
Kwa msimu 2017/2018 Jorginho ndio aliyepiga pasi nyingi katika ligi kuu nchini Italia maarufu kama Serie A akipiga pasi 3198 huku zilizofika kwa mlengwa ni 2861 hii ikiwa ni sawa na 89.68%
Na ndio sababu kubwa ya Sarri alipotua katika klabu ya Chelsea alihitaji huduma ya kiungo huyo kwani msimu 2017/18 hakuna aliyeweza kufikisha pasi alizopiga Jorginho yeye lakini ndio mtu anaeuelewa zaidi mfumo wake.
Mwandishi; Lilian J Mukulu
Mhariri; Barnabas Gwakisa
No comments:
Post a Comment