Klabu ya Chelsea inaweza kumpoteza mshambuliaji wake, Eden Hazard mara baada ya kuripotiwa taarifa kwamba klabu ya Real Madrid imeandaa dau nono ili kumnasa nyota huyo raia wa Ubelgiji.
Taarifa zinadai kwamba klabu ya Real Madrid imeandaa dau la paundi milioni 200 ili kumsajili nyota huyo mwenye miaka 27.
Mlinda mlango wa zamani wa Chelsea, Thibaut Courtois ambaye siku kadhaa zilizopita alikamilisha uhamisho wa kujiunga na Real Madrid anaweza kutumika kama mshawishi kwa mbelgiji huyo mwenzake ambaye mara kadhaa walikuwa wakisema wanatamani kucheza timu moja.
Katika mahojiano ya Courtois toka ajiunga na Real Madrid alisema anatamani kucheza na mbelgiji huyo mwenzake na huenda Madrid wakamtumia kama kishawishi kwa Hazard.
No comments:
Post a Comment