Chelsea inafanikiwa kupata ushindi mnono wa magoli 0-3 ikiwa ugenini ikiibamiza klabu ya Huddersfield. Ushindi unaoifanya kufanikiwa kupanda na kushika nafasi ya kwanza katika msimamo wa ligi kuu Uingereza
Shukrani kwa goli la nyota N'Golo Kante ambaye aliifungia Chelsea goli la kwanza akionganisha pasi iliyopigwa na winga raia wa Brazil ambaye juzi alitoka kutimiza miaka 30, Willian Borges da Silva ambapo.goli hilo linamaanisha kiungo huyo anakuwa mchezaji wa kwanza kuifungia Chelsea goli katika msimu wa 2018-2019 wa ligi kuu Uingereza
Goli la pili lilifungwa na kiungo raia wa Italia mwenye asili ya nchini Brazil mwenye ustadi mkubwa na upigwaji wa pasi zenye ubora uliotimia, Jorginho Frello ambaye alikuwa akiucheza mchezo huu ukiwa kama mchezo wake wa kwanza kwa soka la Uingereza akifunga kwa njia ya penati iliyotokea mara baada ya Marcos Alonso kuchezewa madhambi katika eneo hatari la Huddersfield.
Goli hilo linamfanya kiungo huyo kuwa mchezaji wa nane kufunga kwa penati katika mchezo wake wa kwanza wa ligi kuu Uingereza.
Goli la tatu lilifungwa na winga teleza, Pedro Rodriguez akifunga goli murua akitimiza vyema kazi iliyofanywa na Eden Hazard ambaye aliingia kama mchezaji wa akiba akichukua nafasi ya Willian Borges da Silva.
Kwa ushindi huu unaifanya Chelsea kufikisha alama 3 ikiwa na magoli matatu na kuifanya Chelsea kuwa kileleni mwa ligi kuu Uingereza.
Mchezo unaofata;
Chelsea vs Arsenal
Siku; Tarehe 18-Agosti
Muda; Saa 19:30 (EAT)
Michuano; Ligi kuu Uingereza
Uwanja; Stamford Bridge
No comments:
Post a Comment