Ligi kuu Uingereza; Habari muhimu kuelekea Huddersfield vs Chelsea - Darajani 1905

Ligi kuu Uingereza; Habari muhimu kuelekea Huddersfield vs Chelsea

Share This
Mara baada ya kutambulishwa rasmi kuwa kocha wa Chelsea takribani mwezi mmoja uliopita alipoachana na klabu ya Napoli, kocha Maurizio Sarri jioni ya leo ataiongoza Chelsea kucheza mchezo wake wa kwanza wa ligi kuu Uingereza wakati itakapokuwa ugenini kucheza dhidi ya klabu ya Huddersfield inayoongozwa na kocha David Wagner.

Kuelekea kwenye mchezo huo, hapa nakuletea habari muhimu unazopaswa kuzijua.

Kuhusu mchezo
Ni mchezo wa kwanza wa ligi kuu Uingereza kwa timu zote mbili. Chelsea inacheza mchezo huu siku nne toka ilipocheza mchezo wake wa kirafiki dhidi ya Olympique Lyon, mchezo ulioisha kwa Chelsea kupata ushindi wa matuta (penalty).

Chelsea
Huu ni mchezo wa kwanza kwa kocha Maurizio Sarri, ukiwa ni mchezo wake wa kwanza wa kiushindani ukiachana na michezo mitano iliyopita kama kukipima kikosi chake. Kuhusu majeruhi, Chelsea inaweza kumkosa Cesc Fabregas ambaye alituma picha akiwa hospitalini ambapo inadhaniwa alifika ili kufanyiwa matibabu kutokana na majeraha aliyoyapata kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Arsenal.

Ingawa majeraha hayo hayakuthibitishwa na kocha Maurizio Sarri kwenye mkutano wake hapo jana.

Huddersfield
Wanaweza wakawakosa nyota wao akiwemo Durm na Williams ambao wote wanatajwa kuwa na majeraha.
Utabiri wa Paul Merson
Huddersfield 0-2 Chelsea. Huddersfield watataka kuanza vizuri. David Wagner (kocha wa Huddersfield) alifanya maajabu msimu uliopita kwa kufanikiwa kuibakisha timu ligi kuu walisaidiwa na mwanzo mzuri waliounza. Huu ni mchezo mgumu kwao."
.
"Chelsea wana matatizo yao lakini nafikiri wataanza vyema dhidi ya Huddersfield. Msimu uliopita walienda kucheza dhidi yao na wakafanikiwa kufanya makubwa, nafikiri watataka kuonyesha makubwa wakiwa na kocha wao mpya" alisema mchambuzi wa soka, Paul Merson wakati akiwa anatabiri mchezo wa hii leo kati ya Chelsea dhidi ya Huddersfield ambao leo watakuwa nyumbani.

Mchezo uliopita
Katika mchezo uliopita kwenye uwanja huuhuu, Chelsea ilifanikiwa kuondoka na ushindi wa magoli 1-3, huku Tiemoue Bakayoko akifunga goli kwenye mchezo huu.
Muda
Saa 05:00 Jioni (Saa 17:00) kwa saa za Afrika Mashariki (EAT)

No comments:

Post a Comment